|
|
Ua Kayongo Hybrid Maize
A New Approach to Controlling Parasitic Striga for Kenyan Maize Producers |
|
||||||||||||||||
|
|
Kushirikisha Wakulima Nchini Kenya Kukabiliana na Gugu aina ya Striga
Gugu aina ya striga ambalo hujulikana sana kama Kayongo (Luo) au Oluyongo (Luhya), ni aina ya magugu ambayo pia ni kimelea (hutegemea mimea mingine kukua). Humea na kuharibu nafaka hasa mahindi. Hivyo basi, husababisha ukosefu wa vyakula katika maelfu ya boma. Striga hunawiri vema baada ya kupata chakula chake kutokana na madini ya mimea kama mahindi. Mbegu zake humea kwa urahisi katika mchanga wakati shamba linapolimwa, hivi basi zaweza kubaki kwenye mchanga bila kumea kwa miaka mingi mno. Mbegu zinazomea hujibandika kwenye mizizi ya mimea ya mahindi na hivyo hupata chakula chake kutoka kwa mimea hii. Hali hii husababisha kupooza kwa mahindi kisha kufa. Striga hupaswa kupaliliwa kwa mikono kisha kuchomwa pamoja na mabaki ya mimea iliyomo shambani iliyo adhiriwa na striga. Kuchoma hukomesha kuenea kwa striga.
Aina mpya ya mahindi ya hybrid, iitwayo Ua Kayongo ambayo imepakwa dawa aina ya StrigawayTm ambayo huua magugu, imeletwa sehemu za magharibi mwa Kenya ili kuthibiti kusambaa kwa Striga katika mimea ya mahindi. Dawa hii huua striga ambayo inamea na pia, hujaribu kujibandika kwenye mmea wa hindi. Ua kayongo hupandwa na kusimamiwa kama vile aina zingine za mahindi kwa kufuata utaratibu unaofaa wa kupanda mahindi ya hybrid. Inapaswa kupaliliwa vyema, kupatiwa nafasi bora, mbegu nzuri na hata mbolea, kisha kupalilia na kutoa magugu mara kwa mara. Hata hivyo, mahindi hii ya Ua Kayongo haiwezi kupandwa katika shimo moja na lile lipandwamo maharagwe, kunde na mimea mingine ya sampuli hii (legumes). Ni sharti kwa mkulima kuosha mikono yake vema baada ya kupanda mahindi hii ili kuepuka kupaka mimea mingine dawa hii ya strigawayTm.
Wakulima wanahimizwa kwamba, wanapotumia Ua Kayongo, wanafaa kushirikisha mbinu zingine zinazotumiwa ili kuthibiti kusambaa kwa striga kwa muda mrefu. Wakulima watatambua upungufu wa magugu mengine karibu na miche ya mahindi kwa ajili ya dawa ya StrigawayTm. Mbegu za Ua Kayongo sasa zitaanza kuuzwa katika masoko nchini Kenya. Hii ni kupitia mashirika ya Kenya Seed, Lagrotech na Western Seed. Shughuli hii itaanza mwishoni mwa mwaka huu wa 2005. |
|||||||||||||||||
|
Format Home l Striga Home l Mobilizing Farmers l Striga Threats l Know your Enemy l First Defense Striga Management l Ua Kayongo l Establish Ua Kayongo l Questions on Striga Striga Swahili l Striga Luo l Striga Luhya l Contact Details © 2005.
African Agricultural
Technology Foundation's (
AATF
Striga Management Project ). |
||||||||||||||||||